Ijapokuwa ni vazi, wanawake hawavai vilemba Na hata kama inapendeza, bado hawavai kanzu Hata kunao wengi wasopenda chupi za bambino Nimezaliwa kikamilifu, si nusu kichotara tena ehe Na kama kuku, napenda kula wa afya si mangisi Niliwahi penda vidimu, ila uchachu wake uchungu Na kila uchungu na tamule na kila tamule, tamu Ila mhibu angu, usijigeuze chano watu watakufulia Utamaisi fika simbuko haisimbiki ila kwa msuko Ifanye haramu ya mchwa kuwa bidii yako tena Ili usiishie kuomba kisiki kikukwae upate sababu Na usije kwangu bila haja, aghalabu utanikasirisha Maisha hayana haki kwa wanyonge, wasiojiweza Na tajiri hata na deni, hafai kudaiwa, mkumbushe tuu. |Maisha| #ushairi #life