Nojoto: Largest Storytelling Platform

BADO Menipa hofu ya moyo,kila mi nitembeapo, Nikao

BADO
Menipa hofu ya moyo,kila mi nitembeapo,
Nikaonekana poyoyo,kila mi nisimamapo,
Hadi raha ya kupenda,kwangu imekua chungu,
Siku zote niko macho,silali ja sungusungu,
Ninahisi yangu roho,imejawa na ulungu,
Kifikiri ulienda,nahisi kizunguzungu,
Kesema kweli mwenziyo,roho bado ijapona.

Asante kwa kunumiza,juwa tu ulinifaa,
Wala sitokuuliza,kotini sikati rufa,
Naapa kutolipiza,kwa ngumi wala kifaa,
Yako ushayatimiza,huku roho inanyufa,
Kwa chozi ukaniliza,ningali nakupa sifa,
Mengi kwangu kakatiza,ndoto angu kwako ijafa,
Kusema kweli mwenziyo,roho bado ijapona.

Maneno ya watu sumu,kwa roho ukiamini,
Yamesha nihukumu,nimebaki kulaani,
Pia yamenihujumu,hapo mimi sibishani,
Mulinisema kwa hamu,mebaki bila imani,
Mwanzoni sikufahamu,mtanieka mashakani,
Yeyote simlaumu,mana niko kwa mizani,
Kusema kweli,mwenziyo roho bado ijapona.

Bila we mambo si mseto,nimebaki tu na kero,
Nakuona tu kwa ndoto,usiku mi nilalapo,
Dunia ni janga moto,popote mi niendapo,
Ukaniponda kwa kwato,nimekwama papo hapo,
Insani mejawa kicheko,utadhani kiapo,
Nani ntamtuma kwako,afike uliko?
Kusema kweli mwnziyo,roho bado ijapona.
                                           @fundiflani bado
#Waterfall&Stars
BADO
Menipa hofu ya moyo,kila mi nitembeapo,
Nikaonekana poyoyo,kila mi nisimamapo,
Hadi raha ya kupenda,kwangu imekua chungu,
Siku zote niko macho,silali ja sungusungu,
Ninahisi yangu roho,imejawa na ulungu,
Kifikiri ulienda,nahisi kizunguzungu,
Kesema kweli mwenziyo,roho bado ijapona.

Asante kwa kunumiza,juwa tu ulinifaa,
Wala sitokuuliza,kotini sikati rufa,
Naapa kutolipiza,kwa ngumi wala kifaa,
Yako ushayatimiza,huku roho inanyufa,
Kwa chozi ukaniliza,ningali nakupa sifa,
Mengi kwangu kakatiza,ndoto angu kwako ijafa,
Kusema kweli mwenziyo,roho bado ijapona.

Maneno ya watu sumu,kwa roho ukiamini,
Yamesha nihukumu,nimebaki kulaani,
Pia yamenihujumu,hapo mimi sibishani,
Mulinisema kwa hamu,mebaki bila imani,
Mwanzoni sikufahamu,mtanieka mashakani,
Yeyote simlaumu,mana niko kwa mizani,
Kusema kweli,mwenziyo roho bado ijapona.

Bila we mambo si mseto,nimebaki tu na kero,
Nakuona tu kwa ndoto,usiku mi nilalapo,
Dunia ni janga moto,popote mi niendapo,
Ukaniponda kwa kwato,nimekwama papo hapo,
Insani mejawa kicheko,utadhani kiapo,
Nani ntamtuma kwako,afike uliko?
Kusema kweli mwnziyo,roho bado ijapona.
                                           @fundiflani bado
#Waterfall&Stars
festusogola2386

Festus Ogola

New Creator