Ati akikuomba tuu, unachangamka na kumpatia Na juu hutaki kum'lose, unaamua kujiloosen tuu Wewe, ashaikupatia hata ukimuomba, jijibu tuu Na imagine si ati hana, huyu mtu wako ni mgumu Jipende tuu kidogo aki, kidogo tuu nakuomba. Unajua kuna yule hupewa hata bila kumuomba We nae unashusha points kwa kujipendekeza Ukweli ni ukishamtumia, ni bff huzitoa, akimtoa Na aki ndio Fuliza inakupuliza, utafulizwa wewe Jipende tuu kidogo aki, kidogo tuu nakuomba. Sikatai unampenda, umembuyia data na chats Lakini sasa mbona anakugreytick akiwa online Ukiwa kwake uko flexible, but kwenyu hauko Usiku kwa mchana mko macho, na kanisani? Jipende tuu kidogo aki, kidogo tuu nakuomba. |Jipende| #shairi #love #fakepeople