Nojoto: Largest Storytelling Platform

Tega sikio nikusimulie yangu wewe Kishamba changu

Tega sikio nikusimulie yangu wewe
Kishamba changu kimejilima chenyewe
Vifaranga navyo vikachukuliwa na mwewe
Nimebaki kujifuta machozi mwenyewe

Na vipi kichwani sina hata nywele
Ama ndio msimu wa kupata upele
Usiotibika wa moyoni huu uwele
Nimechoka hata sisongi mbele

Nahisi nafsi yangu imegoma
Moyoni moto nao wanichoma
Inaposambaratika yangu boma
Tabibu wangu yuko Oklahoma
Atakuja niganga nifurahi Obama

Inapunja hisia zangu hali hii kali
Na si ati gharama ya maisha ni ghali
Kwa kuwa nimejimudu kwa kila hali
Ila kwa kuvunjwa, hapa mimi sina mali
Pa kujisetiri hapanijali, ntarudi tu Somali'

|Safari-ya-chozi|
 #pieces
Tega sikio nikusimulie yangu wewe
Kishamba changu kimejilima chenyewe
Vifaranga navyo vikachukuliwa na mwewe
Nimebaki kujifuta machozi mwenyewe

Na vipi kichwani sina hata nywele
Ama ndio msimu wa kupata upele
Usiotibika wa moyoni huu uwele
Nimechoka hata sisongi mbele

Nahisi nafsi yangu imegoma
Moyoni moto nao wanichoma
Inaposambaratika yangu boma
Tabibu wangu yuko Oklahoma
Atakuja niganga nifurahi Obama

Inapunja hisia zangu hali hii kali
Na si ati gharama ya maisha ni ghali
Kwa kuwa nimejimudu kwa kila hali
Ila kwa kuvunjwa, hapa mimi sina mali
Pa kujisetiri hapanijali, ntarudi tu Somali'

|Safari-ya-chozi|
 #pieces
adierpalmer1110

Adier Palmer

New Creator